Ujana ni wakati wa matumaini na wakati wa kufikiria maisha ya kesho, wot e tunataka kuyafurahia maisha yetu na tunataka watu watuheshimu. Kila mmoja ana nia yake ya kufuata; wengine wataka kuwa madkatari,wengine wataka kuoana,wanasheria na hata wanasisa. Lakini matumaini yote tuliyonayo wakati wa kujitayarisha ni sasa.
Vijana tunakazi kubwa sana mbele yetu , kazi hiyo ni kufanya kila tuwezalo kuifanya nchi yetu iwe ni mahali pema pa kuishi.
Kumekua na malalamiko mengi hasai kutoka kwa vijana kuhusu serikali iliyopo madarakani kwamba ni mafisadi, wapendwa rushwa na waroho wa madaraka, hivyo mategemeo yangu kutoka kwa vijana ni kuhakikisha kwamba wanafanya kila litalowezekana kufanyika (kihalali) ili kuondoa matatizo hayo.Nyerere katika hotuba yake ya kwanza ya sherehe ya miaka 10 ya TANU alisema;
"Hii ni mara yangu ya kwanzakuwahutubia watoto na vijana wote wa jamuhuri ya muungano, nami nafurahi kupata nafasi hii. Vijana hamnabudi kujitayarisha sasa kwa maisha yenu ya utu uzima na kuchukua vema madaraka ya nchi hii kutoka kwa wazee wenu”.Lakini mategemeo yangu kwa vijana yaamekua na wasiwasi kwani vijana ambao tummekua tukiwategemea wafanye nchi yetu kuwa mahali pema pa kuishi, wanafanya pawe mahali pa kupachukia na hata kutaka kupakimbia.
Vyombo vya habari vimekua vikiripoti kuhusu migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ambayo imesabisha wanafunzi hao kusimamishwa masomo na wengine kufukuzwa kabisa vyuoni.
Hivi karibuni wanafunzi 48 kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam walifukuzwa kutokana na tatizo hilo la migomo.
Mkuu wa chuo hicho Prof. Makandala alipohojiwa akasema wanafunzi hao wangeweza kukata rufaa au kufanya mazungumzo na sio kufanya mgomo. Aliongeza pia kikao cha 206 cha Baraza la chuo kilichofanyika Desemba 13, mwaka jana, kiliafiki kuwachukulia hatua kali wanafunzi wote walioonekana kuwa vinara wa kuanzisha migomo.
Punde tu kabla ya kuandika taarifa hizi, wanafunzi 13 walifukuzwa chuo na wengine 86 kutoka chuo hicho hicho (chuo kikuu cha Dar es salaam) kusimamishwa masomo baada ya kudaiwa na tuhuma za kuanzisha mgomo chuoni hapo.
Kama hiyo haitoshi Rais na mawaziri wa serikali ya wanafunzi TUSODARCO walikutwa na tuhuma za uchakachuaji wa pesa za serikali hiyo.
Wanafunzi hao hao ambao ni wanaharakati wa taifa lililopo na la kesho ambao wanolalamika na kuilaumu serikali ya Muungano na viongozi wake kwamba ni mafisadi na wapenda rushwa hivyo wamechoka na madhambi ya viongozi hao na hivyo wanaitaji mabadiliko ndio hao hao wanaochakachua pesa za Taasisi zilizopo chini yao kwa matumizi yao binafsi; 'Ama kweli nyani haoni kundule'.
Napenda kusisitiza kwamba, kuhitaji mabadiliko ya nchi hayangoji mpaka ati hapo utakapo kabidhiwa madaraka ya juu ya uongozi Fulani, la hasha, Tabia ni kama ngozi ya mwili. kama umepewa kifursa kidogo tu cha kuwa mwenyekiti/rais au waziri wa serikali ya wanafunzi na punde tu unadaiwa na tuhuma za kuchakachua pesa, je vipi ukipewa uongozi wa kuiongoza nchi yaani kuwa amiri jeshi mkuu?
No comments:
Post a Comment