Wednesday, January 11, 2012

Maafa kutokana na mafuriko.

Mafuriko ni hali ya kuwa na maji mengi yanayofunika nchi kavu pasipo na maji kwa kawaida.

Mafuriko yanaweza kutokea popote baada ya mvua nyingi inayoteremsha maji mengi yasiyo na njia ya kupotea hasa baada ya kutelemka penye mlima au mtelemko. lakini pia mafuriko yanaweza kutokea kando la mto ama baada ya mvua mkali au wakati wa mvua nyingi au kwenye majira ya kuyeyuka kwa theluji.



Mafuriko mara nyingi ni hatari kwa binadamu, huleta hatari kwa maisha, mali na nyumb hivyo kusabisha watu kukosa makazi kwa wakati huo na hata baadae.

Njia za kujiokoa na mafuriko ni pamoja na kuhama haraka penye miinuko au nchi ya juu zaidi; watu waliozoea mafuriko wana mbinu za pekee kama vile kujenga vizuizi vya maji kupanda juu.

kwa maana hiyo, wakazi wote walopoteza makazi yao wamepewa misaada mbalimbali ikiwemo ya kujengewa mahema ili kuishi kwenye mahema hayo.

Mahema hayo yamejengwa kwa misaada ya watu mbalimbali kama vile MSALABA MWEKUNDU na Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa-JKT na JWTZ maeneo ya Mabwe Pande-Bunju B.

Tunashukuru kwamba si haba ndugu zetu wamejengewa mahema ya kuishi na familia zao, lakini ni nini hatma ya watu hao?


 

No comments:

Post a Comment